Friday , 10th Apr , 2015

Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara inatarajia kuendelea kesho katika viwanja vinne tofauti nchini ambapo JKT Ruvu watakuwa wenyeji wa Coastal Union ya jijini Tanga, mechi itakayochezwa Uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam.

Kwa upande wa Kagera Sugar wanatarajia kuwakaribisha maafande wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Kambarage Mjini Shinyanga.

Mjini Morogoro, uwanja wa Manungu Turiani, Timu ya Mtibwa Sugar watawakaribisha Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Azam FC huku Ndanda FC wakiwa wenyeji wa wajelajela Tanzania Prisons ya jijini Mbeya, Mechi itakayochezwa uwanja wa Nangwanda sijaona mjini Mtwara.