Thursday , 2nd Apr , 2015

Timu ya Coastal Union ameanza kuzipigia hesabu pointi tatu muhimu za wapinzani wao Tanzania Prison ili kuweza kuhakikisha wanazichukua wakati watakapokutana kwenye mechi ya Ligi kuu Tanzania bara.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa wikiendi hii kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani ikiwa ni mzunguko wa pili wa ligi hiyo ikielekea lala salama.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo, Afisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kikubwa zaidi wanachojivunia ni kuendelea kuimarika kikosi hicho.

Assenga amesema, mipango mikubwa iliyopo ni kuiwezesha timu hiyo kupata matokeo mazuri katika mechi zote zilizosalia ikiwemo kuwataka wachezaji kutimiza wajibu wao wa kuipa ushindi timu hiyo pamoja na kumaliza ligi hiyo wakiwa nafasi tatu za juu kwenye michuano hiyo ambayo msimu huu imeonekana kuwa na upinzani mkubwa.