Monday , 29th Jun , 2026

Ndani ya saa 24 zilizopita, Iran wamepitia matukio ya kusisimua na ya kuhuzunisha.Walifunga bao la dakika za mwisho dhidi ya Misri na kuamini wamefuzu hatua ya mtoano, lakini baada ya ukaguzi wa VAR, bao hilo lilikataliwa na wakashuka hadi nafasi ya tatu.

Timu ya Taifa ya Iran

Baadaye walilazimika kusubiri matokeo ya mechi nyingine wakitumaini wafuzu kama moja ya timu bora zilizomaliza nafasi ya tatu. kwanza walihitaji Ghana kuifunga Croatia, lakini Croatia ilishinda mchezo huo kwa mabao yaliyopatikana katika dakika za mwisho.

Kisha wakatumaini DR Congo ipoteze au itoe sare, lakini DR Congo iligeuza matokeo na kushinda, tumaini lao la mwisho lilikuwa kwenye mchezo wa Austria dhidi ya Algeria, ambapo walihitaji mshindi apatikane.

Algeria ilifunga bao dakika ya 93 na mashabiki wa Iran wakaanza kushangilia wakiamini wamefuzu. Hata hivyo, dakika ya 96 Austria ilisawazisha, mchezo ukaisha kwa sare na ndoto za Iran zikafikia mwisho