Sheria hiyo inayotarajiwa kuanza kutumika mwanzoni mwa mwaka 2027, huku ukilenga kuwalinda watoto dhidi ya madhara yanayoweza kupatikana kutokana na matumizi ya mitandaoni ya kijamii, na makampuni yatakayokiuka sheria hiyo yatakumbana na faini kubwa.
Lakini cha kushangaza zaidi kwenye hili WhatsApp haitojumuishwa kwenye mitandao itakayofungiwa kwa watoto walio na umri chini ya miaka 16 na hii ni kwa kile wanachodai kuwa inarahisisha mawasiliano ya kifamilia.





