Thursday , 23rd Apr , 2026

Tume iliyoundwa kuchunguza ghasia za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 imetoa ripoti ya inayonyesha kuwa jumla ya watu 518 walipoteza maisha katika vurugu hizo.

 

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othman, amewasilisha takwimu hizo leo Aprili 23, 2026, mbele ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 

“Mkoa wa Dar es salaam ulikuwa na vifo zaidi 182, Mwanza 90, Mbeya 80 na Arusha 53 kati ya vifo hivyo 21 vifo vya Watoto katika kundi hilo 15 walikuwa Watoto wa miaka 15 hadi 17, huku vifo vinne ni kati ya (miaka 7 hadi 10), na wawili ni chini ya umri wa miaka 5’’ alisema Jaji Chande.

 

Ripoti imebainisha kuwa asilimia 96.7 ya waliouawa ni wananchi wa kawaida, huku asilimia 3.1 wakiwa ni watumishi wa vyombo vya ulinzi, Raia 502 na Maafisa wa Usalama 16

 

Ripoti hii inakuja ikiwa ni miezi kadhaa baada ya ghasia za uchaguzi uliopita, Ripoti iliyoleta mapendekezo muhimu na Serikali kuahidi kuendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kujua kiini cha ghasia hizo.