Tuesday , 21st Apr , 2026

Meneja wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger amefunguka kuwa bado Arsenal inayo nafasi ya kushinda ubingwa wa Ligi kuu Uingereza licha ya kupigika weekend iliyopitwa na wapinzani wao Manchester City

Arsene Wenger

"Ninaamini kwamba Arsenal itashinda ligi, Ninaamini kwa dhati, Inaonekana, kwangu, kama akili ya kawaida"

Pia Wenger amefunguka kuwa wachezaji wanaomvutia katika kikosi cha Arsenal ni pamoja na Eze, Odegaard, Havertz na Madueke 

Baada ya Arsenal kusubiri taji la Ligi Kuu  kwa miaka 22 mbio hizo zinaonekana kukaribia mwisho, lakini matokeo ya hivi karibuni yametilia shaka mbio za The Gunners kwenye ubingwa wa EPL

Kufuatia matokeo ya mechi ya wikendi iliyopita kati ya Arsenal na Manchester City , kocha huyo wa zamani wa Gunners ametoa mtazamo unaopinga uwezekano wa mashine ya City kuepukika.