Mwenyekiti wa Bodi ya Simba Crescentius Magori na Inno Loemba
“Kwanza Loemba hajaletwa na JayRutty, alitafutwa na Kamati ya Usajili kwa kushirikiana na kocha".
"Mkataba wa JayRutty ndio unasema atasajili mchezaji mmoja ndio tukamwambia alipie gharama zake za usajili. Kwani Mohammed anavyosajili wachezaji kwahiyo ni wachezaji ni wa Mohammed?
"Mkataba wa JayRutty unasema kila mwaka atasajili mchezaji mmoja hivyo na mwakani mjiandae kuna mchezaji mwingine atalipia gharama za kumsajili".
"Loemba aliumia tangu mechi ya Singida na alianza mazoezi juzi na kocha akamuweka benchi mechi ya Azam. Hakucheza sababu mwalimu aliona bado timu inayocheza ipo vizuri na hakutaka kuchukua risk ya kumchezesha.”




