Serikali ya Korea Kaskazini imeonya kuhusu madhara yatakayojitokeza kufuatia mazoezi ya kijeshi yanayofanywa kwa pamoja kati ya Marekani na Korea Kusini.
Dada wa kiongozi wa nchi hiyo, Kim Yo Jong, alionya kuwa mazoezi hayo kati ya Marekani na Korea Kusini yatachochea vurugu katika eneo hilo, akisisitiza kuwa Korea Kaskazini itaimarisha uwezo wake kukabiliana na vitisho vitakavyojitokeza.
"Kutushiana misuli kunaweza kuleta shida kwahiyo maadui zetu wasitujaribu”, alionya Kim Yo Jong.





