Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Siku ya Wanawake Duniani ni siku muhimu ya kutambua mchango mkubwa wa Wanawake katika mandeleo ya familia, jamii na Taifa kwa ujumla akisema kwa hapa nchini, maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kaulimbiu "Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi wa Kufikia Dira ya Taifa ya Mandeleo 2050," huku kimataifa yakiadhimishwa chini ya kaulimbiu "Give to
Gain" - Kutoa ndiko Kupata.
Rais Samia kupitia ujumbe wake wa Siku ya Wanawake leo March 08,2026, amesema “Kauli mbiu hizo zinatukumbusha kwamba maendeleo ya kwell ya jami na Taifa letu yanajengwa katika msingı wa haki na sawa na ushirikishwaji, pamoia na moyo wa kujitoa, kushirikiana na kuwainua wengine, kwa asili, Mwanamke ni Mama, ni Mlezi, ni Kiongozi na ni Mfariji wa familia, jamii na Taifa.
“Katika maisha ya kila siku, Wanawake wanaishi kwa vitendo falsafa ya "Kutoa ndiyo Kupata", wanajitoa kwa Familia zao, wanalea kizazi, wanahudumia jamii na wanachangia kwa namna mbalimbali maendeleo ya Taifa letu, hata katika nyakati za changamoto, Mwanamke hakimbii majukumu, badala yake, hubeba changamoto hizo kwa ujasiri na hekima, na kuzigeuza kuwa nguvu ya kuimarisha familia, jamii na Taifa.





