Monday , 9th Feb , 2026

Super Star wa muziki duniani Chris Brown anasema ni salama kwa mashabiki zake kusema wanamuhitaji kumuona akiperforme Super Bowl halftime show.

Picha ya msanii Chris Brown

Chris Brown amegusia hilo kupitia 'Insta Story' yake muda mchache baada ya kumalizika show Super Bowl aliyofanya Bad Bunny.

"Nadhani ni salama kusema wananihitaji mimi" amesema Chris Brown

Wiki kadhaa zilizopita zilianza kampeni kutoka kwa wadau wa muziki, mashabiki na wasanii kama Ne-Yo na rapa Boosie Badazz zikisema Chris Brown anatakiwa aperform Super Bowl.