Akizungumza kwenye mahojiano,amesema kuwa kipindi hicho kilikuwa cha changamoto kubwa si tu kwenye muziki bali pia kwenye maisha yake binafsi na afya ya akili. Ameeleza kuwa lawama, maneno ya kukatisha tamaa kutoka kwa umma na shinikizo la mitandao ya kijamii vilimfanya ajitafakari upya kuhusu maisha na mwelekeo wa kazi yake.
Hata hivyo, Meek Mill anasema hakuruhusu hali hiyo kumdhoofisha, bali aliitumia kama somo la kujijenga upya. Kwa sasa, anasema ameweka mkazo zaidi kwenye ukuaji binafsi, biashara, familia na kujenga legacy yake, badala ya kujihusisha na migogoro au drama zisizo na tija.
Kauli ya Meek imewapa matumaini mashabiki wake wengi, ikionyesha kuwa licha ya misukosuko ya umaarufu, msanii anaweza kusimama tena na kuendelea kusonga mbele akiwa na mtazamo mpya wa maisha na kazi.



