Wednesday , 28th Jan , 2026

Mshambuliaji wa Athletic Bilbao, Nico Williams, huenda akakosa nafasi katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kitakachoshiriki Kombe la Dunia 2026, kufuatia jeraha la ‘Pubalgia’ ambalo limeshindwa kupona kwa wakati.

Nico Williams na Lamine Yamal

Taarifa kutoka gazeti la Marca imeeleza kuwa, hali ya mchezaji huyo haiwashawishi madaktari wa klabu yake wala wa timu ya taifa, jambo ambalo limeibua wasiwasi mkubwa kuhusu uwezekano wa kushiriki kwake kwenye mashindano hayo makubwa.

Hata hivyo, kuna uwezekano wa Nico Williams kufanyiwa upasuaji, ambao unaweza kuwa suluhisho pekee la kuhakikisha anapata nafuu.

Wadau wa soka wanangojea kwa hamu uamuzi wa madaktari na klabu, huku matumaini makubwa yakiwa ni kwamba Nico ataweza kurejea uwanjani akiwa tayari kwa mashindano ya kimataifa.