Monday , 19th Jan , 2026

Nahodha msaidizi wa timu ya Taifa ya Senegal Sadio Mane baada ya mchezo wa fainali ya AFCON uliokuwa wa vuta nikuvute amepinga kitendo cha kocha kutoa timu uwanjani akidai kitendo cha "Kijinga"

“Kandanda ni mchezo  wa kipekee, dunia ilikuwa inatazama, hivyo tunatakiwa kutoa taswira nzuri kwa soka.

"Nadhani itakuwa ni ujinga kutocheza mchezo huu kwa sababu mwamuzi alitoa penalti na tunatoka nje ya mchezo, Nafikiri hilo litakuwa jambo baya zaidi hasa katika soka la Afrika. Ni afadhali nishindwe kuliko mambo ya aina hii kutokea kwenye soka letu.

"Nadhani ni mbaya sana, Soka haipaswi kusimama kwa dakika 10 lakini tufanye nini? Lazima tukubali tulichofanya lakini jambo zuri ni kwamba tulirudi na tukacheza mchezo na kilichotokea kilitokea."