Sunday , 11th Jan , 2026

“Hatua zaidi zinachukuliwa dhidi ya mtuhumiwa kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kisheria”

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Joseph Daudi Mwakalinga, mkazi wa Zimbili, Kinyerezi wilaya ya Ilala, Dar es Salaam kwa tuhuma za kumjeruhi kwa fimbo na moto mtoto wake ambaye jina lake limehifadhiwa.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam iliyotolewa leo Januari 11, 2026, Joseph anadaiwa kutenda tukio hilo Januari 8 ambapo alimjeruhi kwa fimbo na moto mtoto wake huyo.

“Hatua zaidi zinachukuliwa dhidi ya mtuhumiwa kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kisheria”, taarifa ya Polisi imeongeza.

Kufuatia tukio hilo, wito umetolewa kwa wazazi, walezi na wananchi kwa ujumla kuepuka vitendo vya ukatili.