Elizabeth Jayunga mwenye umri wa miaka 30 ambaye ni mkazi wa Kitongoji cha Imilamate B, Kijiji cha Tumaini Kata ya Itenka Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi amefariki dunia kwa kupigwa na radi baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kunyesha.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema mvua hiyo ilikuwa na upepo mkali hali ambayo imesabisha kadhia hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amefika eneo la tukio na kutoa pole kwa wahanga wa tukio hilo.
Jamila amewaomba wananchi wa Kijiji hicho kuwa watulivu huku akiiagiza kamati ya Maafa halmashauri ya Nsimbo kuanza kufanya tathimimi ya uharibifu ulitokana na mvua hiyo.
Mvua hiyo iliyoanza kunyesha majira ya saa tisa alasiri, licha ya kusabisha kifo cha mtu huyo mmoja imeezua nyumba zipatazo 30 na makanisa 5.
