Sunday , 28th Dec , 2025

Hii ni mara ya pili kwa mtaa wa Mitendewawa kukumbwa na maafa ya aina hiyo, ambapo mwaka 2024 mwezi Desemba pia nyumba kadhaa zilianguka kutokana na mvua na upepo mkali.

Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mhe. Wilman Kapenjama Ndile, ameutembelea mtaa wa Mitendewawa uliopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, kufuatia maafa ya kuanguka kwa nyumba tisa kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali.

Tukio hilo limetokea tarehe 24 Desemba, 2025, na kusababisha baadhi ya familia kukosa makazi baada ya nyumba zao kuharibika kabisa.

Hii ni mara ya pili kwa mtaa wa Mitendewawa kukumbwa na maafa ya aina hiyo, ambapo mwaka 2024 mwezi Desemba pia nyumba kadhaa zilianguka kutokana na mvua na upepo mkali.

Akizungumza na wananchi wa mtaa huo wakati wa ziara yake, Mhe. Ndile amewapa pole waathirika wa tukio hilo na kuwataka kuchukua tahadhari zaidi, hususan katika ujenzi wa makazi yao.

Amesisitiza umuhimu wa wananchi kujenga nyumba imara kwa kuzingatia viwango na taratibu za ujenzi, ili kupunguza athari za majanga yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.