Monday , 22nd Dec , 2025

Wanachama hao wamelalamikia hatua ya jesho la polisi kukataa kurejesha jengo hilo ili hali walipewa kwa muda wakati wanaandaa jengo la ofisi yao.

Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi ameliagiza jeshi la polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya kupisha jengo linalomilikiwa na Chama kikuu cha wakulima wa Mara WAMACU na ametoa muda wa mwezi mmoja ili kupisha shughuli za uzalishaji wa sekta ya kilimo pamoja na matumizi ya ofisi za ushirika huo.

Kauli yake imefuatia malalamiko yaliyowasilishwa kwake na wananchi wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa 16 wa chama kikuu cha wakulima wa Mara Coopertive WAMACU uliofanyika mkoani Mara ambapo wanachama hao wamelalamikia hatua ya jesho la polisi kukataa kurejesha jengo hilo ili hali walipewa kwa muda wakati wanaandaa jengo la ofisi yao.

Kufuatia malalamiko hayo mkuu wa mkoa wa Mara akatoa maagizo kwa jeshi la polisi kupisha haraka jengo la wakulima ili shughuli za uzalishaji ziweze kuendelea kwa ufanisi.

Wanachama pamoja na viongozi wamezungumzia walivyopokea maamuzi hayo na kusema kuwa jengo hilo litaongeza ukuaji wa uchumi kwa wananchi pamoja na taifa kwa ujumla.