Friday , 28th Nov , 2025

Akisoma uamuzi wa Mahakama hiyo leo, Ijumaa Novemba 28.2025 Jaji Awamu Mbagwa amesema, Mahakama imekubaliana na pingamizi lililokuwa limewekwa na Wakili wa utetezi Hekima Mwasipu kuwa maombi hayo yameletwa Mahakamani hapo nje ya muda.

Maamuzi ya kesi ya kukiuka amri ya Mahakama iliyokuwa inawakabili viongozi wa CHADEMA yametupiliwa mbali na Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam leo Novemba 28,2025.

Maombi hayo Namba 25480/2025 yaliyokuwa mbele ya Jaji Mbagwa yaliletwa na Said Issa na wenzake wakitaka Viongozi wa Chama hicho wakamatwe na kufungwa kwa kukiuka amri ya Mahakama ya tarehe 10 June 2025 iliyotoa katazo la kufanya Mikutano ya Kisiasa.

Viongozi hao walikuwa ni;

1. John Heche

2. John John Mnyika

3. Rose Mayemba

4. Brenda Rupia

5. Hilda Newton

6. Twaha Mwaipaya

7. Gervas Benard Lyenda

8. Board ya Wadhamini

Akisoma uamuzi wa Mahakama hiyo leo, Ijumaa Novemba 28.2025 Jaji Awamu Mbagwa amesema, Mahakama imekubaliana na pingamizi lililokuwa limewekwa na Wakili wa utetezi Hekima Mwasipu kuwa maombi hayo yameletwa Mahakamani hapo nje ya muda.

Jaji Mbagwa amesema kesi ya msingi namba 8960/2025 iliyoko chini ya Jaji Hamidu Mwanga ndio iliyokuwa msingi wa kesi iliyokuwa mbele yake, na kwamba amri ya Mahakama kuzuia shughuli za kisiasa za CHADEMA ilitolewa na Mahakama Juni 10, 2025 na kuongeza kuwa kesi ya kudharau amri ya Mahakama ililetwa Mahakamani hapo Oktoba 03 mwaka huu takribani siku 106 jambo ambalo halikubaliki kisheria, Sheria inataka maombi ya aina hiyo yaletwe ndani ya siku 60.