Mkurugenzi wa Mazingira toka ofisi ya Makamu wa Rais Dr Julius Ningu.
Hayo yamesemwa na Dr Julius Ningu Mkurugenzi wa Mazingira toka ofisi ya Makamu wa Rais katika uzinduzi wa Nishati mbadala itokanayo na takataka za Mazao na wanyama Kwa ajili ya kutumika katika viwanda nchini.
Dr Ningu amesema Taka za mazao kama mapumba ya Mpunga, Mabaki yatokanayo na mbao pamoja na kinyesi cha wanyama huweza kuzalisha Umeme hadi Megawati 650.
Kwa upande wake mratibu wa Mradi wa Nishati toka UNIDO Emmanuel Michael amesema ni wakati sasa kwa Watanzania kujifunza teknolojia hii mpya na rahisi kwenye taasisi zinazotoa mafunzo ya kuzalisha nishati mbadala ili kujipatia Ajira na kuwezesha kukua kwa Viwanda kwa kuwa na umeme wa uhakika.