Wednesday , 17th Sep , 2025

Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro amelazwa katika hospitali ya Brasilia siku ya Jumanne, Septemba 16, 2025, baada ya kujisikia vibaya, siku chache baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 27 jela kwa jaribio la mapinduzi

Akiwa chini ya kifungo cha nyumbani tangu mapema mwezi Agosti, kiongozi huyo wa zamani wa mrengo wa kulia mwenye umri wa miaka 70 (2019-2022) alijisikia vibaya, akiwa katika hali nzito, kutapika na kushuka kwa shinikizo la damu

Rais huyo wa zamani alipatwa na kipindi kikali zaidi cha kizunguzungu ambacho kilimwacha bila kupumua kwa karibu sekunde kumi," baadaye amewaambia waandishi wa habari nje ya hospitali.

Hali ya Jair Bolsonaro mwenye umri wa miaka 70 ni shwari, lakini hajajisikia vizuri, seneta huyo amesema, na kuongeza kuwa baba yake angelala usiku huo "chini ya uangalizi.

Baada ya vipimo, kiongozi huyo wa zamani wa Brazil amepokea dawa kwa njia ya mishipa, mkewe, Michelle Bolsonaro, amesema kwenye Instagram, akiwataka wafuasi wa mumewe kuendelea kumuombea

Siku ya Jumanne mchana, maafisa wa polisi wa gereza walisimama nje ya hospitali hiyo, AFP imeripoti.

Rais huyo wa zamani amepata matatizo mengi ya kiafya katika miaka ya hivi karibuni na amefanyiwa upasuaji mara kadhaa kutokana na athari za shambulio la kisu alilopata wakati wa umati wa watu wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2018.

Mnamo mwezi Aprili, alifanyiwa upasuaji mkubwa wa tumbo uliochukua zaidi ya saa kumi na mbili ili kutatua kizuizi cha matumbo. Kisha alikaa hospitalini kwa wiki tatu ili kuweza kupata nafuu.