Monday , 28th Jul , 2025

Marekani na Umoja wa Ulaya zimekubaliana kushusha ushuru kwa bidhaa za Ulaya hadi asilimia 15 kutoka asilimia 30 iliyowekwa mwanzoni na Rais wa Marekani, Donald Trump

Marekani na Umoja wa Ulaya zimekubaliana kushusha ushuru kwa bidhaa za Ulaya hadi asilimia 15 kutoka asilimia 30 iliyowekwa mwanzoni na Rais wa Marekani, Donald Trump

Trump na Rais wa Kamisheni ya Ulaya, Ursula von der Leyen, wametangaza makubaliano hayo nchini Scotland jana Jumapili Julai 27, baada ya mkutano uliodumu kwa saa nzima.

Trump hakusita kusifia uwekezaji wa Umoja wa Ulaya wa dola bilioni 600 ndani ya Marekani na ongezeko kubwa la ununuzi wa nishati vifaa vya kijeshi kutoka Marekani na ameyaita makubaliano hayo kuwa makubwa kabisa kuwahi kufikiwa.

Rais wa Kamisheni ya Ulaya, von der Leyen amekiri kuwa Trump ni mtu mgumu kuafikiana naye, na amesema wao kama Umoja wa Ulaya, aslimia 15 ndicho kitu pekee walichofanikiwa kukipata.