Saturday , 19th Jul , 2025

Kwenye moja ya Podcast ambayo msanii davido amefanya siku za hivi karibuni amefunguka kuwa Tajiri namba moja duniani (Kwa watu wote wenye asili ya Afrika) Aliko Dangote ni Baba yake wa ubatizo na kujisifia kuwa yeye yupo vizuri (Kiuchumi)

Katika podcast hiyo pia Davido ameweka wazi kuwa ushauri ambao kila siku anapokutana na na Dangote jambo pekee ambalo huwa anaambiwa ni kuhakikisha anatunza pesa/anatumia pesa vizuri

Kitu kingine pia ambacho kiliwashangaza watangazaji zaidi ni baada ya Davido kuwambia kuwa Baba yake huyo wa ubatizo ana zaidi ya miaka 10 hajawahi kununua gari jipya kwaajili ya matumizi yake"Anaendesha gari ya mwaka 2005" na ni zaidi ya miaka 20 hajawahi kwenda Vacation"