
Mombasa ni miongoni mwa majimbo 21 yaliyoathiriwa na mlipuko huo, ambapo maambukizi ya kwanza eneo hilo yalithibitishwa Septemba mwaka jana.
Mkurugenzi wa huduma za matibabu wa kaunti Dk Mohamed Hanif amewaambia wanahabari kuwa kuna maambukizi mengi eneo la Mombasa kwa sababu jamii haijakubali kuwa ugonjwa huu upo
Dk Mohamed Hanif amesema Wagonjwa wengi wana umri wa kati ya miaka 24 na 45. Mtoto mdogo zaidi ana umri wa miaka 12. Sote tuko hatarini,” alisema Dk Hanif.
Kufikia mwisho wa wiki, tangu mwaka jana, Mombasa ilikuwa imerekodi maambukizi 98 yaliothibitishwa na vifo viwili. Wakaazi wengi wamechanganya vipele vya Mpox kuwa hali nyingine kama vile ugonjwa wa ndui au vipele vya joto.
Tangu Kenya kutangaza mlipuko wa Mpox tarehe 31 Julai 2024, Wizara ya Afya imethibitisha maambukizi 226 na vifo vinne nchini kote. #EastAfricaTV