Friday , 20th Mar , 2015

Mchezaji wa Kimataifa anayechezea Klabu ya Simba, Daniel Sserunkuma anatarajia kujiunga na kambi leo akitokea nchini Uganda ambapo aliomba ruhusa kwa ajili ya kwenda kumaliza matatizo ya kifamilia.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Stephen Ally amesema, Mganda huyo anatarajia kujiunga na wenzake kambini kwa ajili ya kujiandaa na muendelezo wa michuano ya mechi za Ligi kuu Soka Tanzania Bara ambapo Simba itawakaribisha Ruvu Shooting Jumapili, Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Ally amesema, katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting watamkosa Golikipa Ivo Mapunda ambaye licha ya kuwa na kadi nyekundu aliyeipata katika mechi dhidi ya Mgambo JKT ya jijini Tanga lakini anasumbuliwa na tatizo la jicho.