
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamsaka mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Mgore anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 na mkazi wa lbanda, Kata ya Kirumba Wilaya ya llemera kwa tuhuma za mauaji ya mume wake aitwaye Amosi Faustine Paulo, miaka 31, dereva wa pikipiki na mkazi wa lbanda aliyeuawa kwa kukatawa na kitu chenye ncha kali kichwani upande wa kisogoni.
Tukio hilo limetokea Juni 25,2025 majira ya saa 4.30 usiku huko katika hospitali ya Mkoa wa Mwanza, Sekou-Toure muda mchache wakati Amosi Faustine Paulo alipofikishwa kwa ajili ya kupatwa matibabu ili kuokoa maisha yake baada ya kujeruhiwa na kitu chenye ncha kali na mke wake wakiwa chumbani kwenye nyumba ya Joseph Bukoma Misungwi iliyo eneo la lbanda, Wilaya ya llemera walipokuwa wamepanga.
Jesh la Polisi linaendelea na uchunguzi sambamba na kumsaka mtuhumiwa aliyetoroka baada ya kutenda tukio hilo ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria. Mwili wa marehemu umefanywa uchunguzi wa kitakalamu na kukabidhiwa ndugu kwa taratibu za mazishi. Aidha, chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi kwani inadaida mwanamke huyo alikuwa akimtuhumu mume wake kuwa na mahusiano ya kimaezi na wanawake wengine.