Thursday , 26th Jun , 2025

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Ruangwa Mkoani Lindi Mhe. Kassjm Majaliwa Majaliwa amewashukuru wananchi wa Jimbo la Ruangwa kwa kuendelea kumuunga mkono na kumpa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake, akiwajulisha kuwa atarejea tena kwenye kinyang'anyiro

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Ruangwa Mkoani Lindi Mhe. Kassjm Majaliwa Majaliwa amewashukuru wananchi wa Jimbo la Ruangwa kwa kuendelea kumuunga mkono na kumpa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake, akiwajulisha kuwa atarejea tena kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge katika Jimbo hilo.

Mhe. Majaliwa amebainisha hayo leo Alhamisi Juni 26, 2025, Bungeni Mjini Dodoma, wakati akiwasilizha hotuba ya kuhitimisha mkutano wa 19 wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,akimshukuru pia Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake na maelekezo yenye tija, yaliyoifanya kazi yake kuwa nyepesi.

"Ninatambua wakati mwingi nimekuwa nje ya jimbo nikilitumikia taifa lakini wana Ruangwa wameendelea kuniunga mkono. Nitumie nafasi hii kusema asanteni sana na ninamuomba Mwenyezi Mungu azidi kuimarisha mshikamano uliopo kati yetu sote. Ninaomba kuwajulisha kuwa ninakuja kuchukua fomu ya kuomba ridhaa yenu tena." Amesema Waziri Mkuu.