
Abby alikuwa ni Muafrika mashariki pekee aliyepata nafasi ya kuwania tuzo hiyo ambapo pamoja na kukosa tuzo hiyo (Best International Act) bado Wanaafrika mashariki wameendelea kumuonesha upendo na sapoti.
Kupitia Insta yake Abby amepost ujumbe wenye maana yakuwa......."Hii imekuwa sura ya kuvutia sana. Nimeguswa kwa dhati na upendo na msaada niliopokea kutoka kwa nchi yangu na hata zaidi. Nasonga mbele nikiwa na furaha moyoni na moto rohoni, huu ni mwanzo tu.''
Abby anaingia kwenye rekodi ya Watanzania Wachache kama Alikiba,Diamond,Rayvanny ambao wamewahi kupata nafasi ya kuchaguliwa kuwania tuzo za kimataifa kama BET na nyingine nyingi