
Pichani Nandy na Yammi
"Hakunipigia simu kiukweli kwahiyo nilimtafuta kwenye DM (instagram) kwasababu ni sehemu anayopenda kuingia sana, kwahiyo nilimtumia hiyo interview nikamuuliza umenipigia simu siku mbili zipi mbona sijaona simu?'' Amesema Nandy
"Nikamwambia pia kama ulinipigia simu na hukunipata una namba ya mdogo wangu,ya dada yangu ana namba hadi ya Naya (Mtoto wa Nandy) angeweza kunitafuta kote huko kama sipatikani lakini kiukweli kwenye simu yangu Mungu ananiona sikuona Simu yake" Amesema Nandy
"Lakini yeye alichonijibu ni kwamba aliibiwa simu hakuwa na namba na mara ya mwisho mimi ndio nilimpigia akaniambia aliibiwa vitu vyake kwahiyo kwake yeye ilitokea namba lakini mimi nilivyompigia hakuniambia kama ana uzinduzi inawezekana labda alikuwa bado hajapanga uzinduzi'' Amesema Nandy