Tuesday , 13th May , 2025

Hii leo itapigwa michezo minne ya Ligi Kuu ya NBC katika Viwanja tofauti tofauti, JKT Tanzania watacheza dhidi ya Fountain Gate, Ken Gold dhidi ya Pamba Jiji, Yanga SC dhidi ya Namungo Fc huku Azam Fc watachuana dhidi ya Dodoma Jiji Uwanja wa Chamazi.

Kagera Sugar na Pamba Jiji

Baada ya Kagera Sugar kupoteza mchezo wa Ligi hapo jana Uwanja wa nyumbani kwa goli 1-0 dhidi ya Mashujaa, kikosi hicho kimesalia nafasi ya 15 kwa alama 22 tofauti ya alama 5 dhidi ya Pamba Jiji wenye alama 27 nafasi ya 14 eneo la  PlayOffs.

Endapo Pamba Jiji wakashinda mchezo wa leo dhidi ya Ken Gold watafikisha alama 30 ambazo hazitoweza kufikiwa na Kagera Sugar hata akishinda michezo yake miwili iliyosalia Namungo Fc pamoja na Simba Sc atafikisha alama 28.

Fountain Gate wanashika nafasi ya 13 eneo la PlayOffs wakiwa na alama 29, kwa tafasiri hiyo Kagera Sugar wanaweza kushuka daraja hii leo na kuungana na Ken Gold kuelekea Championship msimu ujao.