Monday , 12th May , 2025

Zaidi ya watu 100 wamefariki kufuatia mafuriko katika kijiji kimoja karibu na fukwe za Ziwa Tanganyika, huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Picha ya mafuriko DRC

Hayo yameelezwa na msimamizi wa wilaya ya Fizi katika mkoa wa Kivu Kusini  Samy Kalodji, ambaye ameeleza kwamba mafuriko hayo yameathiri kijiji cha Kasaba ambako taarifa zinaonesha kwamba zaidi ya watu 100 wamekufa.
 
Mafuriko hayo yanashuhudiwa kwenye eneo hilo katika wakati ambapo mashambulizi ya waasi wa M23 yameongezeka katika eneo hilo la Mashariki tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Maelfu ya watu waliuwawa katika kipindi cha miezi miwili ya mwanzo mwa mwaka huu, kufuatia mapigano hayo.