Saturday , 10th May , 2025

Mshambuliaji  wa Liverpool Mohamed Salah ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa 2024-2025 zinazotolewa na  Chama cha waandishi wa habari za soka. 

Mohamed Salah - Mshambuliaji  wa Liverpool

Salah amefunga mabao 28 na kutoa asisti 18 zilizoisaidia  Liverpool kushinda taji la EPL  na kuweka  rekodi ya kuhusika kwa mabao mengi katika mechi 38 za msimu mmoja  wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Salah alishinda kwa asilimia 90 ya kura zilizopigwa na zaidi ya wanachama 900 wa FWA, na hivyo kuufanya ushindi huo kuwa ushindi mkubwa zaidi katika karne hii akimshinda mchezaji mwenzake wa Liverpool Virgil van Dijk mshambuliaji wa Newcastle Alexander Isak na kiungo wa Arsenal Declan Rice aliongia nao top 4.

Katika hatua nyingine mshambuliaji wa Arsenal Alessia Russo ameshinda tuzo hiyo kwa upande wa wanawake akimshinda  mshindi wa mwaka jana Khadija Shaw na kuwa mchezaji wa pili wa Arsenal kushinda tuzo hiyo.