Wednesday , 30th Apr , 2025

Rais wa Marekani, Donald Trump ameadhimisha siku ya 100 ya muhula wake wa pili ofisini na hotuba ya mtindo wa kampeni, akishabikia mafanikio yake na kulenga maadui wa kisiasa.

Akiangazia kile alichokiita mapinduzi ya akili ya kawaida, aliwaambia umati wa wafuasi huko Michigan kwamba alikuwa akitumia urais wake kufanya mabadiliko makubwa.

Chama cha Republican kilimdhihaki mtangulizi wake wa chama cha Democratic, Joe Biden, na kuanzisha ukosoaji mpya kwa mwenyekiti wa Benki Kuu ya Marekani, huku akitupilia mbali kura za maoni ambazo zinaonyesha umaarufu wake unashuka.

Utawala wa Trump umehakikisha idadi ya wahamiaji haramu wanaoingia Marekani kinyume cha sheria inapungua lakini uchumi unaweza kuwa hatarini kisiasa huku akianzisha vita vya kibiashara duniani.

Akizungumza katika kitovu cha sekya ya magari Marekani, Trump alisema kampuni za magari zinajipanga kufungua viwanda vipya vya utengenezaji katika jimbo la Midwestern.
Katika mkutano wake wa hadhara, Trump pia alisema kura za maoni zinazoonyesha umaarufu wake umeshuka ni feki.