Tuesday , 29th Apr , 2025

Kocha Hansi Flick anatarajia kusaini mkataba mpya Barcelona hadi Juni 2027. Flick amefanya mapinduzi makubwa Barcelona tangu alipowasili majira ya joto yaliyopita ikiwemo kuchukua ubingwa Super Cup Spain na Copa del Rey kufuatia kufukuzwa kwa Xavi Hernandez.

Kocha wa Barcelona Hansi Flick

Licha ya kutofautiana mitizamo miezi michache iliyopita kuhusu hatma yake inatajwa kuwa uamuzi huo umefanywa na rais Joan Laporta na bodi ya wakurugenzi.

Flick alisaini mkataba wa miaka miwili baada ya kuwasili Catalonia, lakini katika wiki za hivi karibuni kumekuwa na mazungumzo kuhusu yeye kuongeza mkataba.

Barcelona na Flick wamefikia makubaliano ya kuongeza mkataba kwa msimu mmoja zaidi pamoja na wakufunzi wake, watapokea nyongeza ya mishahara kama sehemu ya mkataba huu mpya, ambao utatangazwa mwisho wa msimu huu.