Tuesday , 29th Apr , 2025

Mkuu wa idara ya usalama wa ndani Israel, Shin Bet, Ronen Bar, ametangaza kuwa atajiuzulu Juni 15, wiki sita baada ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kujaribu kumuondoa.

Bar ataacha wadhifa wake takriban miezi 18 kabla ya mwisho wa muda wake ulioratibiwa, akikubali kuwajibika kwasababu ya shirika lake aliloongoza Shin Bet, kushindwa kuzuia shambulio la Oktoba 7, 2023.

Baada ya miaka 35 ya utumishi, na kuruhusu utaratibu mzuri wa kuteua mrithi wa kudumu na mpito wa kitaaluma, nitamaliza majukumu yangu mnamo Juni 15, 2025," Barr alisema katika taarifa.

Bar alikuwa mmoja wa wapatanishi wakuu wa Israeli katika mazungumzo ya kusitisha mapigano na kuwaachilia mateka.

Shin Bet imekuwa kiini cha vita vya kisiasa vinavyozidi kuongezeka kati ya serikali ya mrengo wa kulia ya Netanyahu na kundi la wakosoaji wake, kuanzia wanachama wa taasisi ya usalama hadi familia za mateka wanaoshikiliwa huko Gaza.

Makabiliano hayo yalifichua mgawanyiko mkubwa katika siasa za Israel na jamii kati ya mrengo wa kulia, unaomuunga mkono Netanyahu, na warengo huria zaidi wa nchi hiyo, ambao wameingia mitaani kupinga hatua za serikali za kuweka mipaka ya mamlaka ya mahakama kwa miezi kadhaa.

Bar ilikuwa imewasilisha ombi la kufutwa kwazi kwake, jambo ambalo liliigawa Israel na kusababisha kuibuka kwa masimulizi yanayokinzana kuhusu matukio ambayo yalisababisha shambulio lisilokuwa la kawaida la Hamas mnamo Oktoba 7, 2023