Monday , 28th Apr , 2025

Mtu mmoja ambaye jina lake halijafahamika anayekadiriwa kuwa na miaka 35 jinsia ya kiume amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unaelea kando ya mto Mpanda eneo la Misunkumilo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi. 

Mwili

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Idaya Makoroboyi na Edesi Mlango wamesema kuwa tukio hilo ambalo sio la kawaida limewashitusha wakazi wengi wa Mtaa wa Mpanda Hotel

Ibrahim Msanda Mwenyekiti wa mtaa wa Mpanda Hotel amesema kuwa alipata taarifa hiyo kutoka kwa mjumbe wa serikali ya mtaa.

Emanuel Ndochi Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto mkoa wa katavi amesema wamefika eneo la tukio na kufanya uokozi wa mwili wa marehemu kwenye Mto huo