
Akizungumza na mwandishi wa habari aliyehoji kwamba Kyiv ilikubali pendekezo la Marekani la kusitisha mapigano kabisa Machi 11, lakini Moscow iliweka masharti.
Bwana lavrov alijibu: "Hapana, haya sio masharti,". "Haya ni masomo ambayo tumejifunza angalau mara tatu, wakati mikataba inayofanana na tunayojadili sasa ilihitimishwa"
Lavrov amesema kwamba kwa usitishaji mpya wa mapigano nchi za Magharibi lazima ziache kuipatia Ukraine silaha.
Kyiv na washirika wake wa Ulaya hapo awali waliita hali hii kuwa haikubaliki, kwani Ukraine ingekuwa bila ulinzi mbele ya mchokozi.
Kulingana na Lavrov, Ulaya ilisema moja kwa moja kwamba inaweza tu kuunga mkono makubaliano ambayo hatimaye yataifanya Ukraine kuwa na nguvu zaidi, ambayo itaifanya Ukraine kuwa mshindi.