
Tundu Lissu
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA Brenda Rupia na kueleza kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA John Heche, anatarajiwa kufika gereza la Ukonga leo kwa ajili ya kumwona Lissu na kuzungumza naye kuhusu hali yake.
"Kufuatia taarifa hiyo, familia, wanachama wa CHADEMA na Watanzania wote waliokuwa na wasiwasi kuhusu mahali alipo Mheshimiwa Lissu, wanataarifiwa kuwa sasa wanaweza kumtembelea kwa kufuata taratibu za kawaida za kumuona mahabusu katika gereza hilo," imeeleza taarifa hiyo