
Klabu ya Paris Saint-Germain
PSG wametangazwa kuwa mabingwa bila kupoteza mchezo wowote mpaka sasa msimu huu wakiwa wamecheza michezo 28 wakishinda michezo 23 na kutoa sare katika michezo 5 wakiwa wamebakiza michezo 6 ili kukamilisha michezo 34 ya msimu huu.
Bao la pekee la Doue dakika ya 55 ya mchezo akimalizia pasi ya Kvaratskhelia limetosha kuwapa ubingwa huo wa kwanza baada ya kuondoka kwa Kylian Mbappe.
NB: PSG imekuwa timu ya kwanza kutangaza ubingwa msimu huu kwa Ligi tano bora Barani Ulaya.