
Thomas Muller - Nyota wa Bayern Munich
Taarifa hiyo imetoka hii leo baada ya Bayern Munich na nyota huyo mwenye umri wa miaka 35 kukubaliana kutoongeza mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia The Bavarians baada ya miaka 25 ya kuwa pamoja
Bingwa huyo wa treble mara mbili alijiunga na Bayern Munich 2000 katika timu ya vijana akiwa na miaka 10 na kupandishwa katika kikosi cha kwanza miaka 8 baadae na anaondoka katika klabu hiyo akiwa na mataji 12 ya Bundesliga na mataji mawili ya UCL
Kiungo huyo mshambuliaji ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi ndani ya kikosi hiko akiwa amecheza michezo 743, magoli 247 na assist 273