Tuesday , 25th Mar , 2025

Kwa mujibu wa Mwananchi Newspaper Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi amepanga kukutana viongozi wa Shirikisho la Soka la nchini (TFF), Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) na Klabu ya Yanga ili kutatua mgogoro unaoendelea

Kwa mujibu wa Mwananchi Newspaper Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi amepanga kukutana viongozi wa Shirikisho la Soka la nchini (TFF), Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) na Klabu ya Yanga ili kutatua mgogoro unaoendelea kuhusu kusogezwa mbele kwa mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

 

“Ni kweli tutakutana na Waziri Kabudi kuhusu masuala mbalimbali, ikiwemo kusogezwa mbele kwa mchezo wetu dhidi ya Simba. Tumepokea barua na tutahudhuria,” alisema afisa mmoja wa Yanga aliyeomba kutotajwa kwa jina.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa alithibitisha kikao hicho kitafanyika jijini Dar es Salaam, Alhamisi ya Machi 27 kikiongozwa na Waziri Kabudi.

 

Msigwa pia alieleza maofisa wa Simba watashiriki katika kikao hicho ili kupata ufumbuzi wa mchezo wa Kariakoo dabi uliokuwa umepangwa kufanyika Machi 8 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, kisha kuahirishwa baada ya Simba kudai makomandoo wa Yanga waliwakatalia kuingia uwanjani kwa ajili ya mazoezi yao ya kabla ya mchezo.