Friday , 7th Mar , 2025

Liverpool wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kuhitaji huduma ya mshambuliaji wa Newcastle United Alexander Isak.

Alexander Isak - Mshambuliaji wa Newcastle United

Isak yuko nyuma ya Erling Haaland na Mohamed Salah pekee katika orodha ya wafungaji bora wa Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu, amefunga mabao 19 na kukifikisha idadi yake ya mabao 50 katika mechi 76 tangu ajiunge na kikosi hicho kwa pauni milioni 63 mwaka 2022.

Huku Newcastle wakiwa na hofu ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao, kumekuwa na uvumi mkubwa kwamba Isak anaweza kutaka kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto licha ya kuwa na mkataba hadi 2028,

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta anajulikana kuwa shabiki mkubwa wa Isak mwenye umri wa miaka 25, wakati Chelsea na Barcelona zote zimekuwa zikihusishwa na kumtaka. Liverpool pia wanakutaka kufanya mazungumzo huku ikitajwa atagharimu pauni milioni 150 kuondoka Newcastle.