
''Tunawaambia wafanyakazi wetu pindi wanapokuja kujiunga na kampuni hii na kuwakumbusha mara kwa mara kwamba ni kinyume na sera za kampuni kuvujisha siri za kampuni, haijalishi ulikuwa na nia gani
Hivi karibuni tulifanya uchunguzi ambao ulibaini uwepo wa wafanyakazi wetu zaidi 20 ambao wamesambaza taarifa za siri kuhusu kampuni yetu, na tunatarajia kuendelea na uchunguzi na kubaini wengine zaidi na tutachukua maamuzi kwa kila ambaye atabainika na uvujishaji wa taarifa'' - Taarifa ya META kwa umma
Haya yanajiri mara baada ya uwepo wa taarifa za ndani ya kampuni hiyo kuvuja taarifa ambayo ilihusisha kikao cha mkurugenzi wa kampuni hiyo Mark Zuckerberg. META wanaweka mkazo kwa kusema kwamba haitokuwa na msamaha kwenye kosa la namna hiyo.