Tuesday , 25th Feb , 2025

Mlinzi wa Chelsea Wesley Fofana amerejea katika kikosi hiko baada ya kukaa nje ya uwanja takribani miezi miwili akiuguza jeraha la paja alilolipata Disemba 2024 katika ushindi wa 3-0 walioupata Chelsea dhidi ya Aston Villa

Wesley Fofana - Beki wa klabu ya Chelsea

Ikumbukwe mwanzoni mwa mwezi Januari kocha wa Cheslsea Enzo  Maresca alisema Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 24 anaweza kukosekana mpaka mwishoni mwa msimu na kuwafanya  The Blues  kuamua kumrejesha Trevoh Chalobah kutoka Crystal Palace kama mbadala wa Fofana . 

Chalobah raia wa Uingereza anakabiliana na jeraha dogo ambalo litamfanya akose mchezo dhidi ya watakatifu Southampton Utakaopigwa leo saa 5 Usiku  huku  Fofana anatarajiwa kuwepo kwenye kikosi hiko