
Robin Van Persie - Kocha mpya wa Klabu ya Feyenoord
Van Persie ambaye aliwahi kuwa mshambuliaji wa Arsenal na Manchester United anaenda kuiongoza klabu hiyo inayoshika nafasi ya 4 katika msimao wa Eredivisie akichukua nafasi ya Brian Priske aliyeondoka klabuni hapo wiki iliyopita
Feyenoord inakua timu ya pili kwa Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 41, tangu aanze rasmi kibarua cha ukocha 2024 akiwa na Heereveen inayoshika nafasi ya 9 katika msimamo wa ligi kuu nchini Uholanzi
Ikumbukwe Feyenoord ilikuwa klabu ya kwanza kwa Robin Van Persie kuichezea katika soka la kulipwa mwaka 2001 kabla ya kutimkia Arsenal na alistaafu soka lake la kulipwa klabuni hapo mwaka 2019.