
Pichani ni Marioo na Paula
Marioo ameeleza hayo baada ya kuhudhuria katika harusi ya marafiki zao Hamisa Mobeto pamoja na Mchezaji mpira wa klabu ya Yanga mwenye asili ya Bukinafaso Aziz Ki
Marioo ameweka wazi matamanio yake hayo kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo amepost video akiwa na mpenzi wake na kisha kuandika.....''Nimepata Mshawasha wa kuoa Wallah'' jambo ambalo limewaaminisha mashabiki wa watu hawa Marioo na Paula kuwa huenda wakakutana ndoa siku za hivi karibuni