
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Aidha Pia Waziri Mkuu Majaliwa amezungumzia kuhusu ukatili wa teknolojia, akisema kuvujisha picha za mtu za faragha, kuvujisha mitandaoni taarifa binafsi za watu pamoja na kusambaza picha za kubuni zenye kufanana na uhalisia ni miongoni mwa mambo mengine yenye kuhesabika kama makosa ya ukatili wa kijinsia.
Waziri Mkuu pia ambaye amekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni hiyo, amekemea tabia za kushusha heshima na thamani ya mtu, kuita watu majina mabaya, kumuaibisha mtu, lugha za matusi, fedheha pamoja na tamaduni za utakaso zinazofanywa na baadhi ya jamii kwa akinamama wajane ambao hutafutiwa waume na baadhi ya ndugu wa marehemu pale mume wake anapotangulia mbele za haki.