Saturday , 15th Feb , 2025

Waziri wa mambo ya Nje wa Djibouti Mohammed Ali Youssouf anasubiria kutangazwa rasmi kama mrithi wa Moussa Faki Mahamat baada ya kuibuka mshindi kwenye kinyang'anyiro kikali dhidi ya wagombea wa Kenya na Madagascar.

Waziri wa mambo ya Nje wa Djibouti Mohammed Ali Youssouf anasubiria kutangazwa rasmi kama mrithi wa Moussa Faki Mahamat baada ya kuibuka mshindi kwenye kinyang'anyiro kikali dhidi ya wagombea wa Kenya na Madagascar.

Baada ya raundi saba za upigaji kura, Mgombe kutoka Kenya Raila Odinga alijiondoa kwenye kinyang'anyiro alipopata matokeo ya chini.

Safari ya aliyekuwa Waziri Mkuu nchini Kenya Raila Odinga kuwa Mwenyekiti wa Tume ya AUC inafikia kikomo rasmi licha ya taifa lake wakiongozwa na Rais William Ruto kumpigia kampeni kali.

Kinyanga'anyiro hicho kimekuwa kigumu huku wajumbe wakipiga kura kwa araundi saba, bila ya mshindi wa moja kwa moja kupatikana.

Raundi ya sita ya kura hizo zilikutanisha wagombea wawili tu Odinga na ambapo matokeo yalikuwa Djibouti walipata kura 26 na Kenya ilipata kura 22 na kwenye raundi ya 7 ambayo Odinga alijitoa mgombea wa Djibouti amejizolea kura 33.

Ni siku chache tu zilizopita mwanasiasa huyo maarufu wa siasa za upinzani Kenya alisema kuwa iwapo atashindwa atakubali kushindwa na atarudi kwao nchini Kenya kwani hajafukuzwa "Kura itapigwa Jumamosi hii inayokuja, mimi naenda, nikichaguliwa sawa na nisipochaguliwa sawa. Sivyo? Si mimi niko na nyumbani kwetu?” alisema Odinga