Thursday , 13th Feb , 2025

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeipiga tena kalenda, Kesi namba 35738/2024 inayomkabili mfanyabiashara Vicent Masawe maarufu kama ‘baba harusi aliyejiteka’, kwakuwa upelelezi wake bado haujakamilika

Vicent Masawe (36), Mfanyabiashara

Kesi hiyo imetajwa kwa mara ya katika Mahakamana ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi, Ana Magutu kwa niaba ya Hakimu Nyaki ambaye yupo likizo kwa sasa, mwendesha mashtaka ambaye pia wakili wa Serikali Cathbert Mbilinyi amesema upelelezi wa Kesi hiyo bado haujakamilika huku akiiomba Mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa. Aidha kufuatia ombi hilo Hakimu Magutu akatoa muda kwa upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi na kuiahirisha kesi hiyo mpaka Machi 12,2025.

 

Masawe anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni wizi wa gari aina ya Toyota Ractis lenye thamani ya Sh15 milioni ambalo aliazimwa kwa ajili ya kulitumia katika sherehe ya harusi yake na pia kujipatia fedha taslimu Sh3 milioni kwa njia ya udanganyifu.

 

Katika shtaka la kwanza la wizi wa kuaminika, Masawe anadaiwa kuwa akiwa wakala, Novemba 15, 2024 katika Jiji la Dar es Salaam, aliiba gari lenye namba za usajili T 642 EGU aina ya Toyota Ractis.

 

Masawe anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni wizi wa gari aina ya Toyota Ractis lenye thamani ya Sh15 milioni ambalo kwa mujibu wa upande wa mashtaka ni mali ya Silvester Masawe. Na shtaka la pili ni la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, anadaiwa kuwa tarehe hiyohiyo katika Jiji la Dar es Salaam, kwa lengo la kuiba na kutapeli, alijipatia fedha taslimu Sh 3 milioni kutoka kwa Silvester.

 

Kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tena Machi 12,2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.