![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2025/02/06/37LBf5vB5w0Qpjec3ux0dYgcRiZNdixWiN1uLvog.jpg?itok=f0jXU9yo×tamp=1738859298)
Akithibisha kutokea kwa tukio hilo, mkurugenzi wa shule za bressing modern, mwalim Ezekiel Mollel. Amesema watoto hao waliotekwa ni wanafunzi wa darasa la kwanza na mwingine darasa la pili.
Tukio hilo la kusikitisha limezua taharuki na hofu kubwa Kwa jamii wakiwemo wazazi wa watoto hao, ambapo wameliomba jeshi la polisi mkoani Mwanza kusaidia watoto hao ili wapatikane wakiwa hai.
Jeshi la polisi mkoani Mwanza limethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo limeanza kufanya uchunguzi wa kina ikiwemo kufuatilia nyendo za watekaji ili kuhakikisha watoto hao wanapatikana wakiwa salama.
Pamoja na uchunguzi unaoendelea kufanywa na jeshi la polisi watekaji hao wamekuwa wakituma jumbe kwa mkurugenzi wa shule hiyo wakishinikiza kupewa fedha ili kuwaachia huru watoto hao.