Friday , 31st Jan , 2025

"Suala alilozungumzia ni nyeti mno, suala la akina mama na mambo mengine ya dharula tunatoa maelekezo mahususi kwanza moja kwa hospital za private lakini pia za umma kwamba mama na mtu mwingine yoyote wa dharula kwamba kwanza apate huduma sio suala la kuuliza fedha

"Suala alilozungumzia ni nyeti mno, suala la akina mama na mambo mengine ya dharula tunatoa maelekezo mahususi kwanza moja kwa hospital za private lakini pia za umma kwamba mama na mtu mwingine yoyote wa dharula kwamba kwanza apate huduma sio suala la kuuliza fedha, ni kwamba huduma kwanza mambo mengine baadaye lakini niwaambie waheshimiwa wabunge kwenye hili eneo la akina mama na watoto tunajua sisi wenyewe tumepitisha Bilioni 200 kwa ajili ya dawa lakini ukipiga gharama za mwaka za kutibu akina mama na watoto kwa mwaka ni Bilioni 227 na sisi tumetenga kwa huduma zote ni Bilioni 200 kwahiyo kunakuwa na hatua mbali mbali zinafanywa ili kubalance hizo hela"

"Na tunao watu wengi kule lakini unakuta mtu huyo huyo hana bima hana chochote lakini anachangia Milioni kwenye harusi, lakini ikifika suala la mke wake kujifungua hana hizo fedha anataka aseme asaidiwe bure kwahiyo wabunge naombeni muendelee kutuvumilia lakini mjue serikali kwa mwaka juzi tu ilitumia Bilioni 661 kwa eneo tu la msamaha kwahiyo serikali imekuwa ikifanya hivyo lakini tukubaliane wote kupanga ni kuchagua"

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akijibu swali la Mbunge wa viti Maalumu, Anatropia Lwehikila Theonest juu ya kauli ya Serikali kuhusu wanawake wanaoshindwa kupata vifaa vya kujifungua na viongozi ambao wanatoa kauli za kuwakatisha tamaa wanawake hao leo bungeni.